explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya mikono miwili katika sijida ya swala, nayo ni kwa kuviweka vizuri viganja vyake katika ardhi na aviweke vidole vikiwa vimefungamanishwa kuelekea kibla, na viwe viwiko viwili -maungio ya mkono na muundi wake- viwe vimenyanyuka na viko mbali na kugusa Ardhi, na vimeachanishwa na mbavu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Jambo la wajibu kwa mwenye kuswali ni kuweka viganja vyake juu ya Ardhi, na viganja viwili ni viungo katika viungo saba vya kusujudu.
  • Ni sunna kunyanyua miundi ya mikono isiguse Ardhi, na machukizo ya kuilaza kama anavyolaza mnyama mkali mikono yake.
  • Sheria ya kuonyesha uchangamfu na nguvu na hamu katika ibada.
  • Mwenye kusali akiegemea viungo vyake vyote vya kusujudu, kila kiungo kitachukua haki yake katika ibada.