Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa tabaka bora la watu waliokusanyika katika zama moja ni tabaka ambalo yuko ndani yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, kisha wale wanaowafuata katika waumini wale waliowapata Maswahaba na hawakumpata Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wale wanaowafuata nao ni wafuasi wa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapata wasi wasi swahaba katika kutaja wale wanaowafuata kwa karne ya nne. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika baada yao kuna kizazi (kaumu) watafanya hiyana na wala watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi kabla ya kutakwa kutoa ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na wanachupa mipaka katika ulaji na unywaji mpaka unadhihiri kwao unene.