explain-icon

Ufafanuzi

Anamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya hivyo pasina haki, atakuwa ametenda kosa kubwa na dhambi miongoni mwa madhambi makubwa, na atakuwa kastahiki kemeo hili kali.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Tahadhari kubwa ya waislamu kuwapiga ndugu zao waislamu.
  • Katika maovu makubwa na ufisadi mkubwa katika ardhi ni kutangaza silaha dhidi ya waislamu, na kufanya ufisadi kwa mauaji.
  • Kemeo lililotajwa halihusiani na kupigana kwa haki, kama kuwapiga waliokengeuka na mafisadi na wengineo.
  • Uharamu wa kuwatisha waislamu kwa silaha au kinginecho hata kama ni kwa sura ya mzaha.