explain-icon

Ufafanuzi

Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumwambia Mundhiri bin Aidhi, Ashajji ni kabila la Abdil-Kaisi na yeye ndiye alikuwa mtemi wao radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Hakika kwako kuna sifa mbili anazipenda mno Mwenyezi Mungu, nazo ni: Akili, kuhakiki mambo, na utulivu, na kutokuwa na pupa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kujipamba na upole utulivu.
  • Himizo la kuhakiki mambo na kutazama mwisho wake.
  • Upole na utaratibu ni miongoni mwa sifa nzuri.
  • Mwenyezi Mungu Mtukufu humsifia mtu kwa sifa alizomuumba nazo miongoni mwa tabia njema.
  • Ashajju: Ni mtu aliyejeruhiwa usoni, au kichwani, au katika paji la uso.