Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.