Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kudumu kuisoma Qur'ani; kwa sababu itawatetea wasomaji wake wenye kuifanyia kazi siku ya Kiyama, kisha akatilia mkazo katika kusoma sura mbili, Baqara na Al-Imrani, ameziita kuwa ni mapambo mawili yenye kung'aa; kwa sababu ya nuru yake na muongozo wake, na kwamba malipo na thawabu za kuzisoma na kuzingatia maana zake, na kuyafanyia kazi yaliyomo, haya yatakuja siku ya Kiyama kama mawingu mawili, au kinginecho, au kama makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao walioungana baadhi yao kwa baadhi, zikimkinga msomaji wake na zikimtetea. Kisha akatilia mkazo rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Suratul-Baqara na kuzingatia maana zake na kuyafanyia kazi yaliyomo, na kwamba hilo lina baraka na manufaa makubwa ndani yake katika dunia na Akhera, na kuliacha hilo kuna masikitiko na majuto siku ya Kiyama, na kwamba miongoni mwa fadhila za sura hii nikuwa wachawi hawawezi kumdhuru mwenye kuisoma.