Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake baadhi ya tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwa zile alizozieleza: Nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kupewa hiyari baina ya mambo mawili isipokuwa alichukua jepesi zaidi kati ya hayo, madamu hilo jepesi halipelekei katika madhambi, basi alikuwa akijiweka mbali zaidi kuliko watu wote, na hapo anachagua gumu zaidi. Hakuwahi kulipiza kisasi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake binafsi, bali alikuwa akisamehe na kufuta katika haki yake isipokuwa yakivunjwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu hapo analipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na alikuwa ni mtu mwenye hasira kuliko watu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.