Alituma Jeshi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akamfanya bwana mmoja katika Maanswari kuwa kiongozi wao, na akawaamrisha wamtii, yule kiongozi akawakasirikia na akasema kuwaambia: Hivi hakuwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Hasa! akasema: Basi nimekuamrisheni nikusanyieni kuni na muwashe moto kisha muingie humo, wakakusanya kuni na wakawasha moto, walipotaka kuingia humo, wakaanza kutazamana wao kwa wao. Na wakasema: Hakika sisi hatukumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake ila ni kwa sababu ya kuukimbia moto, je, tuuingie? wakiwa bado wako katika hali hiyo muwako wa moto ukazimika, na ikatoweka kwa kiongozi ghadhabu yake. Akaelezwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo akasema: Lau wangelimtii na wakaingia katika moto waliouwasha basi wangeliadhibiwa humo na wasingetoka kamwe kwa muda wa kubakia dunia, hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi muumba; bali utiifu ni wajibu katika mambo mema na si katika maasi.