Alimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni wa umma, au sekta binafsi, na akawaingizia tabu na hakuwahurumia, kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kutokana na matendo yake, kwa kumtia matatizo na yeye. Nakuwa atakaye wahurumia na wakawafanyia wepesi, na akawarahisishia mambo yao basi Mwenyezi Mungu naye amuhurumie na ampe wepesi katika mambo yake.