Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume muislamu katika kikoi chake, nacho ni kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume, kwa hali tatu: Ya kwanza: Inayopendeza iwe kati kati ya muundi. Ya pili: Inayojuzu pasina karaha ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili; nayo ni mifupa miwili iliyotokeza katika maungio ya muundi na mguu. Ya tatu: Iliyoharamishwa, nayo ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili, na inahofiwa kwake kupatwa na adhabu ya moto, na ikiwa ni kwa kiburi na kwa kufurahia na ujeuri, Mwenyezi Mungu hatomtazama.