explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Makusudio ya hariri ni hariri halisi ya asili, ama hariri ya bandia ya viwandani haihusiki hapa katika hadithi.
  • Katazo la kuvaa hariri kwa wanaume.
  • Katazo la kuvaa hariri linahusu kuivaa na kuitandika.
  • Wanaume wanaruhusiwa kutumia hariri katika nguo ila isizidi kiwango cha vidole viwili mpaka vinne, itakayofanywa kama mchoro au urembo wa nguo.