Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.