explain-icon

Ufafanuzi

Amepiga mfano Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wa aina mbili za watu: Aina ya kwanza: Rafiki mwema anayemjulisha rafiki yake kwa Mwenyezi Mungu na yanayomridhisha, na kumsaidia katika utiifu, Mfano wake ni kama muuza miski, ima atakupa, au utanunua kwake, au utapata na kunusa harufu nzuri kutoka kwake. Aina ya pili: Rafiki na swahiba mbaya; Anayeziba njia ya Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika kutenda maasi, na unaona wazi kwake matendo machafu, na wewe unasemwa vibaya kwa kufuatana naye na kukaa na mtu kama yeye. Mfano wake ni kama mhunzi apulizaye moto wake; ima itachoma nguo zako kutokana na cheche zake zinazoruka, au utasikia harufu mbaya kwa kukaa karibu naye.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Inaruhusiwa kutumia mifano ili kusogeza maana karibu kwa msikilizaji.
  • Himizo na hamasisho kwa watu kuwa pamoja na watu watiifu na waadilifu, na kujiepusha na watu waovu na wenye maadili mabaya.