Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kupuuza katika kuyafanya madhambi madogo, na kuyakithirisha kwani yanaangamiza yanapokuwa mengi, na akapiga mfano juu ya hilo wa watu walioshuka chini ya bonde, basi akaja kila mmoja wao na kijiti kidogo, mpaka wakaivisha mkate wao kwa mkusanyiko wa vile walivyovikusanya katika vijiti, na hakika madhambi yadharauliwayo pindi anapohesabiwa mfanyaji wake na akawa hajatubia kutokana na madhambi hayo au Mwenyezi Mungu amsamehe, basi humuangamiza.