Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ilikuwa katika muongozo wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi na anayapokea; kwa sababu ni mepesi kubebeka na yana harufu nzuri.
Katika Faida za Hadithi
Inapendeza kukubali zawadi ya marashi; kwa sababu hakuna tabu kuyabeba kwake na wala hakuna masimango ikiwa mtu atayakubali.
Ukamilifu na tabia njema za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kutokataa marashi, na kukubali zawadi ya yeyote mwenye kumzawadia.