Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yake kwenda Yemen kwa ajili ya kuwafundisha watu na kuwafikishia ujumbe, na miongoni mwa yale aliyomuamrisha achukue kutoka kwa Waislamu zaka za ng'ombe zao katika kila ng'ombe thelathini achukue dume moja au ng'ombe aliyeanza kufuatana na wengine machungani; naye ni yule aliyetimiza mwaka moja, na katika kila ng'ombe arobaini achukue ng'ombe mkamilifu; naye ni yule aliyetimiza miaka miwili. Na achukue jizia (kodi) kutoka kwa watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwa kila mwanaume aliyebalehe, Dinari, au kinacholingana na Dinari katika nguo za Yemen ziitwazo: Maafari.