explain-icon

Ufafanuzi

Aliulizwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake, na alikuwa akifanya nini? Akasema: Alikuwa ni mtu kama watu wengine, na anafanya wanayofanya wanaume katika majumba yao, anashughulika na kujihudumia yeye na familia yake; anakamua mbuzi wake mwenyewe, na anashona nguo yake, na anashona kiatu chake, na anatengeneza ndoo yake, na ulikuwa unapofikia wakati wa kusimamishwa swala anatoka kwa ajili yakusali rehema na amani ziwe juu yake bila kuchelewa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ukamilifu wa unyenyekevu wake rehema na amani ziwe juu yake na wema wake kwa familia yake.
  • Amali za kidunia hazitakiwi kumshughulisha mja akawacha swala.
  • Kuhifadhi kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala, mwanzo wa wakati wake.
  • Amesema bin Hajari: Na hapa kunahimizo la kuwa mnyenyekevu na kuacha kiburi na mwanaume kuihudumia familia yake.