Ameeleza Umaima binti Ruqaiqa radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alimuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na wanawake wa ki Answari (watu wa Madina) wampe ahadi ya utiifu juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala wasiibe, na wala wasizini, na wala wasilete uzushi watakaouzua mbele ya mikono yao na miguu yao, na wala wasimuasi katika jema lolote, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Katika yale mnayoyaweza, na mkayamudu. Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kweli, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kukupa mkono kama wanavyofanya wanaume, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali kauli yangu na kukubali kwangu kuungwa mkono na wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja.