Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa haitakiwi kwa muislamu anapokuwa na kitu cha kutolea usia katika haki au mali hata kama ni ndogo, alale siku tatu, isipokuwa ahakikishe usia wake umeandikwa kwake. Akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Sikuwahi kulala hata usiku mmoja tangu nilipomsikia rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa nilikuwa nikikaa na usia wangu.