Aliomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mtoa rushwa na mchukuaji wake na mpokeaji wake. Na miongoni mwake ni kile kinachotolewa kwa mahakimu ili wapindishe hukumu wanayoisimamia; ili mtoaji aitumie kama njia ya kufikia lengo lake pasina haki.