Walikuwa miongoni mwa Mayahudi wa Madina ni Bani Kuraidha na Bani Nadhiri, na kabila moja lilikuwa limelitenza nguvu na kulishinda kabila jingine katika zama za ujinga, wakaridhiana na wakapatana kuwa kila mtu aliyeuliwa na mtu mtukufu mwenye nguvu katika madhalili waliozidiwa basi fidia yake ni Waski hamsini tu (kg 6,100), na kila maiti mtukufu aliyeuliwa na mtu dhalili basi fidia yake ni mara mbili, Waski mia moja (kg 12,200) na waski moja ni sawa na vibaba sitini. Walikuwa katika utaratibu huo mpaka alipokuja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuhama, na makundi yote mawili yakajishusha kwa kufika kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, naye rehema na amani ziwe juu yake kwa wakati huo alikuwa bado hajapata ushindi dhidi ya maadui zake, na hajawatenza nguvu ili wamtii; kwa sababu hilo lilikuwa mwanzoni mwa kuhama kwake, na ilikuwa kipindi cha mkataba wa maridhiano (Hudaibia). Kabila dhalili mtu mmoja akamuua mmoja katika watu watukufu, kabila tukufu wakatuma ujumbe kwa watu dhalili: Yakuwa tutumieni Waski mia moja kama makubaliano yalivyokuwa tangu awali, kabila dhalili likasema: Je, linawezekanaje hili katika mitaa miwili, dini yao moja, na nasaba yao moja, na mji wao mmoja, halafu fidia ya baadhi yao iwe nusu ya wenzao?!, hakika sisi tulikupeni fidia hii kwa kutudhulumu, na kwa kuwahofu, ama kwakuwa Muhammadi amekuja hatutokupeni fidia hiyo milele. Vita vikakaribia kuwaka baina yao, kisha wakaridhiana kuwa wamfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakimu kati yao, kisha kabila tukufu likatafakari, wakasema: Wallahi Muhammadi hatokupeni kutoka kwao mara mbili ya kile atakachowapa wao, na hakika wamesema kweli, hawakutupa kiwango hiki isipokuwa kwa dhuluma, na kwa kuwatenza nguvu, tumeni watu kwenda kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa siri watakaokuleteeni mtazamo wake, ikiwa atakupeni mnachokitaka basi mfanyeni kuwa hakimu, na asipokupeni mnachotaka achaneni naye na wala msifanye kuwa hakimu baina yenu. Wakatuma watu kwa siri kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika wanafiki ili wajue mtazamo wake rehema na amani ziwe juu yake, walipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Mwenyezi Mungu akateremsha wahyi na akamueleza Mtume wake kuhusu swala lao lote na walichokitaka, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika suratul Maida kwanzia kauli yake: "Ewe Mtume, wasikuhuzunishe wale wanaokwenda mbio katika kukupinga, miongoni mwa wale waliosema tumeamini" [Maida: 41]. Mpaka katika kauli yake: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47]. Kisha akasema bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yao: Kwa makundi hayo mawili Wallahi ndio iliteremka kauli yake Mtukufu: "Na asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri" [Maida: 44], na "...basi hao ndio madhalimu" [Maida: 45] na "...basi hao ndio mafasiki" [Maida: 47], na hao hakika ndio aliowakusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.