Ameeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, yakwamba alikuwa amekaa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsikia mtu mmoja akisema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitawanywesha maji mahujaji. Na mwingine akasema: Na mimi sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na akasema mwingine: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio bora zaidi kuliko hayo mliyoyasema. Omari bin Khattwabi akawakemea kwa kunyanyua sauti zao mbele ya Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na tukio hilo lilikuwa asubuhi ya siku ya Ijumaaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika haya mliyotofautiana kwayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Mnayafanya yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuamirisha msikiti mtukufu ni kama imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Haziwi sawa hali za Waumini na hali za makafiri mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaelekezi watu wanaozidhulumu nafsi zao kwa ukafiri kwenye mambo mema." [At-Tauba: 19].