Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema wakati wa kuzidi kwa matatizo na huzuni kwake: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Mtukufu" wa cheo, Mtukufu wa shani, katika dhati yake na sifa zake na majina yake, "Mpole" asiyemharakisha mwenye kuasi kwa kumpa adhabu bali anaichelewesha, na anaweza kumsamehe pamoja nakuwa anauwezo wa kumuadhibu, yeye ndiye muweza Mtukufu juu ya kila kitu ni muweza. "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Arshi tukufu" Muumba wa Arshi tukufu, "Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" na muumba wa mbingu na ardhi, na muumba wa kila kitu ndani yake na mmiliki wake na mrekebishaji wake, na mwenye maamuzi ndani yake kwa namna yoyote aitakayo, "Mola wa Arshi karim" Muumba wa Arshi karim.