explain-icon

Ufafanuzi

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kufanya ibada na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu nyakati za fitina; kwa ajili ya kujilinda na fitina, na kujihifadhi na ufisadi.
  • Kumebainishwa fadhila za kufanya ibada nyakati za fitina na nyakati za watu kughafilika.
  • Inapaswa kwa muislamu ajitenge mbali na mazingira ya fitina na kughafilika.