Ami yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake Al-Abbas bin Abdul Muttalib Allah amuwie radhi alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamfundisha amuombe Mwenyezi Mungu afya njema na salama kutokana na balaa na kasoro za Dini, Dunia na Akhera, akasema: Baada ya siku chache nikarejea kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa mara nyingine tena nikimuomba anifundishe dua nimuombe Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake akimwambia kwa mapenzi na upole: Ewe Abbas, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya aondoe madhara yote na alete kheri na manufaa katika Dunia na Akhera.