Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu ili kujikatia haki ya muislamu, kwani malipo ya hilo ni kustahiki moto, na kunyimwa pepo, nalo ni katika madhambi makubwa. Bwana mmoja akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Hata kikiwa kilichoapiwa ni kitu kidogo? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hata kikiwa ni kijiti cha mswaki unaochukuliwa kutoka katika mti wa Araki.