Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufuga mbwa, isipokuwa kwa haja ya kuwinda, au kulinda mifugo na mazao, na atakayemfuga pasina haja hizo zitapungua katika thawabu za matendo yake kila siku shehena mbili; ambazo ujazo wake unajulikana mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.