Alieleza Abuu Thaalaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa wao wamepewa mtihani wa ujirani wa watu wa kitabu, na makusudio ya hao ni mayahudi na wakristo, je ni halali kwao wale katika vyombo vyao pamoja na dhana ya unajisi wake? Akamjibu kuwa inafaa kula ndani yake, Na ni bora zaidi kuvitumia katika matumizi yasiyokuwa kula kwa sharti mbili: 1- Kutopatikana vyombo vingine tofauti na hivyo. 2- Na wavioshe. Na akamueleza kuwa wao wako katika ardhi ya mawindo, nakuwa yeye anawinda kwa upinde wake na kwa mbwa wake aliyefunzwa juu ya uwindaji na adabu zake, na kwa mbwa wake ambaye hajafunzwa, ni kipi kinachofaa kwake na cha halali katika viwindwa vya hivi vifaa? Akamjibu kuwa alivyoviwinda kwa upinde wake basi hivyo ni halali, kwa sharti ataje jina la Mwenyezi Mungu -Mtukufu- wakati wa kurusha mshale. Na ama unavyoviwinda kwa mbwa, wakiwa wamefunzwa na ukataja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kumtuma hicho ni halali pia, na ama ambao hawajafunzwa, si halali viwindwa vyake isipokuwa atakapokikuta mtu kikiwa hai na akichinje kichinjo cha kisheria.