Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Muislamu atakapotaka kuingia Msikitini amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusema: Allaahumma swalli alaa Muhammadi, kisha aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako". Na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na shetani aliyelaaniwa", na katika riwaya nyingine ya imamu Hakim: Na aseme: "Awe Mwenyezi Mungu nilinde na Shetani aliyelaaniwa".