Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu anapofanya kazi yoyote hata kama ni kuchukua kamba, akaitumia kukusanyia kuni juu ya mgongo wake, akaziuza na akapata chakula kwa hilo, au akatoa sadaka, na akajitosheleza na kutowaomba watu na akaulinda uso wake na udhalili wa kuombaomba; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu, ima wampe au wamnyime, kuwaomba watu ni udhalili, na muumini anaheshima na wala si dhalili.