Alifariki Zainab binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaingia rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake waliotakiwa kumuosha, akasema: Muosheni kwa maji na Mkunazi kwa witiri mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, na muweke katika muosho wa mwisho chochote katika kafuri, na mkimaliza nijulisheni. Walipomaliza kumuosha wakampa idhini, akawapa waoshaji kikoi chake, na akasema: Mzungushieni ndani yake na muifanye kuwa ndio nguo inayofuata mwili wake, kisha kikafanywa kichwa chake kuwa na mafungu matatu ya nywele.