Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika sisi tunapanda majahazi Baharini kwa ajili ya uvuvi au safari za kibiashara na mfano wa hayo, na tunabeba katika safari zetu maji kidogo katika maji yanayofaa kunywa, endapo tukiyatumia maji ya kunywa kwa udhu na kuoga basi yatamalizika, na hatutoweza kupata maji ya kunywa, je, inafaa kwetu sisi tutawadhe kwa maji ya Bahari? Akasema rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji ya Bahari: Maji yake ni safi na yanaweza kusafisha kitu kingine; yanafaa kutawadha na kuoga, na ni halali kula vinavyotoka humo kama samaki na nyangumi na vinginevyo hata kama vitapatikana vimekufa na vinaelea juu yake pasina kuvuliwa.