Aliagiza Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kipande cha dhahabu kutoka Yemen, kikiwa katika ngozi iliyolowekwa na kukwanguliwa, na dhahabu ilikuwa haijapembuliwa kutoka katika udongo wake, akasema: Akaigawanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya watu wanne: Uyaina bin Badri Al-Fazaari, na Aqrau bin Haabisi Al-Handhwali, na Zaidul-Khaili Al-Nab-haani, na Alqama bin Ulaatha Al-Aamiry, bwana moja katika Maswahaba zake akasema: Sisi ndiyo tulikuwa na haki zaidi kuliko hawa, akasema: Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Hivi hamna imani na mimi hali yakuwa mimi ni muaminiwa wa aliyembinguni, zinanijia mimi habari za mbinguni asubuhi na jioni." Anasema: Akasimama mtu mmoja mwenye macho madogo, yaliyoingia ndani ya kope zake, mwenye mashavu makubwa, na mwenye paji refu lililotokeza, na ndevu zake ni nyingi lakini si ndefu, mwenye kipara, na kikoi chake kiko juu upande wa chini wa mwili wake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mche Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Koma!, hivi kwani mimi si mtu mwenye haki zaidi kwa viumbe wa ardhini kumuogopa Allah?!". Anasema: Kisha yule bwana akaondoka, akasema Khalidi bin Walidi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi ni kwa nini nisikate kichwa chake? Akasema: Hapana, huenda akawa anaswali, Khalidi akasema: Kwani wa ngapi wanaoswali lakini wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwa mioyoni mwao?, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi sikuamrishwa kutoboa nyoyo ili kutazama yaliyoko ndani ya nyoyo za watu, wala kupasua matumbo yao; bali nimeamrishwa nichukue yale yanayodhihiri katika mambo yao, akasema: Kisha akamtazama yule akiwa kampa kisogo, akasema: Hakika watatoka watu kutoka katika kizazi cha huyu au kabila lake, watu mahiri katika kusoma kitabu cha Allah, tena kwa sauti nzuri, ndimi zao saa zote ni mbichi kwa wingi wa kukisoma kwake, lakini Qur'ani haivuki koo zao nyoyo zao zikaifahamu ikazitengeneza, na wala Mwenyezi Mungu hainyanyui wala haikubali Qur'ani hiyo wasomayo, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu kama utokavyo mshale katika upinde, kwa kasi na wepesi. Na ninadhani alisema: Nikifika kuwa hai wakati wanatoka dhidi ya waislamu kwa mapanga nitawaua kifo kibaya kama kaumu ya Thamudi.