Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akielezea kukatika kwa Wahyi na kuzuiwa kushuka kwake mwanzo wa kutumwa kwake: Wakati nikiwa natembea katika mitaa ya Makka ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, mara ghafla Malaika Jibril aliyenijia kule pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikapata hofu na fadhaa kwa sababu yake, nikarudi kwa familia yangu nikasema: Nifunikeni kwa nguo. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe uliyejifunika nguo" uliyejigubika kwa nguo zako, "simama" kwa ajili ya kufikisha ujumbe "Uonye" na umtahadharishe asiyeamini utume wako. "na Mola wako Mlezi" Mungu wako muabudiwa "Umtukuze" na umhimidi na umtukuze. "Na nguo zako" na mavazi yako "yasafishe" yaondoshe najisi, "na machafu" kama kuabudu masanamu na mizimu "ihame" iache, Wahyi ukawa na nguvu baada ya hapo na ukakithiri.