Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.