Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa muislamu atakapomuomba Mwenyezi Mungu na akamuomba maombi ambayo si dhambi, kama kumuomba amrahisishie maasi na dhulma, na wala akawa hakuomba kukata udugu; kama kuwaombea dua mbaya watoto wake au ndugu zake wa karibu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwa dua yake hiyo moja kati ya mambo matatu: Ima amharakishie dua yake na ampe alichoomba. Na ima Mwenyezi Mungu amcheleweshee mpaka siku ya Kiyama kwa kumpa daraja za juu zaidi, na rehema na msamaha kutokana na madhambi. Na ima amkinge katika dunia na mabaya mfano wake kwa kiwango cha dua. Maswahaba wakasema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hivyo tukithirishe dua; ili tuweza kupata moja kati ya fadhila hizi? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni mengi na ni makubwa kuliko mnavyoviomba, kipawa chake hakimaliziki, na wala hakiishi.