Alijitahidi Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akawachoma watu fulani kwa moto, miongoni mwa mazandiki walioritadi kutoka katika Uislamu, zikamfikia taarifa Abdallah bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, akamuunga mkono kwa kuwauwa kwake; lakini akakemea kuwachoma kwa moto. Na akasema: Lau ningelikuwa katika nafasi yake nisingeliwachoma kwa moto; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake alibainisha kuwa haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa moto, lakini inatosha tu kuwauwa, kwani alisema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu na akabadili dini yake kwa dini nyingine basi muuweni.