Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni". Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
explain-icon

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona mtu mmoja watu wamemkusanyikia na wamemzingira ili kumkinga na joto la jua na wingi wa kiu, akasema: Kapatwa na nini? Wakasema: Anaswaumu, akasema: Si katika wema kufunga safarini, Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumebainishwa wepesi wa Uislamu.
  • Inafaa kufunga safarini, na pia inafaa kuchukua ruhusa ya kula.
  • Inachukiza kufunga safarini ikiwa ataelemewa, madam hali haitomfikisha katika maangamivu.
  • Amesema Nawawi: Si katika wema nyinyi kufunga mkiwa safarini: Maana yake: Ikiwa swaumu itawapa tabu juu yenu na mkahofia madhara, na mlolongo wa hadithi unaashiria maana hii.
  • Kuwatilia umuhimu Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake na kuuliza kwake hali zao.
explain-icon

Aina tofauti

explain-icon

Ziada