explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa na mkazo mkubwa katika swala za sunna zaidi ya jinsi alivyozikazia na kuzipupia na kuzihifadhi rakaa mbili za sunna ya kabla ya Alfajiri.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Sunna za swala ni zile zisizokuwa faradhi katika ibada, na makusudio yake hapa: Ni sunna zilizopangilia zinazofuatana na faradhi.
  • Sunna zilizopangiliwa: Rakaa mbili kabla ya Alfajiri, na rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili baada ya Ishaa.
  • Sunna ya Alfajiri huswaliwa nyumbani na safarini, tofauti na sunna za Adhuhuri na Magharibi na Ishaa, hizo haziswaliwi isipokuwa nyumbani.
  • Sunna hii imetikiliwa mkazo ya rakaa mbili za Alfajiri, haitakiwi kuzipuuza.