Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa damu ya Muislamu ni haramu, isipokuwa akifanya moja katika mambo matatu: La kwanza: Akatakayetumbukia katika uchafu wa zinaa, na hali yakuwa ameoa ndoa sahihi ya kisheria; ni halali kumuua kwa mpiga mawe. La pili: Atakayeua nafsi isiyo na hatia kwa makusudi pasina haki, atauwawa kwa sharti zake. La tatu: Mwenye kutoka katika umoja wa Waislamu; ima kwa kuacha dini yake ya Uislamu yote kwa kuritadi, au mwenye kutoka bila kuritadi kwa kuacha sehemu ya dini kama waasi, na vibaka, na wanaopiga vita Waislamu kama Makhawariji na wengineo.