explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa sharti bora kabisa kwa kutekelezwa ni zile zilizokuwa sababu ya uhalali wa kustarehe na mwanamke, nazo ni zile sharti za halali anazozitaka mwanamke wakati wa kufunga ndoa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Uwajibu wa kutekeleza sharti ambazo amezitilia umuhimu mmoja kati ya wanandoa wawili kwa mwenzie, isipokuwa sharti itakayoharamisha halali au kuhalalisha haramu.
  • Kutekeleza sharti za ndoa kumetiliwa mkazo kuliko sharti zote; kwa sababu huambatana na kuhalalisha tupu.
  • Ukubwa wa nafasi ya ndoa katika Uislamu, kiasi ambacho umetilia mkazo juu ya kutimiza sharti zake.
explain-icon

Ziada