explain-icon

Ufafanuzi

Alikuja kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika jiwe jeusi katika kona ya Kaaba akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama mimi nisingelimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hapa kuna sheria ya kulibusu jiwe jeusi kwa wenye kuizunguka Al-Kaaba pale wanapolifikia, ikiwezekana hilo kwa wepesi.
  • Makusudio ya kulibusu jiwe jeusi ni kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Amesema Nawawi: Maana yake nikuwa halina uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, nakuwa hilo ni jiwe lililoumbwa kama viumbe vingine ambavyo havidhuru wala havinufaishi, na akalitangaza wazi hilo Omari katika msimu; ili wakashuhudie waliohudhuria katika miji yao, na walihifadhi toka kwake hilo waliohudhuria katika msimu, wanaotoka katika nchi mbali mbali.
  • Ibada zote zinasimama katika msingi wa sheria; haifanyiki katika ibada hizo ila ile aliyoiweka Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa ni sheria.
  • Ikithibiti ibada kuwa ni sahihi itatekelezwa hata kama hekima yake haikujulikana; kwa sababu watu kuitekeleza na kutii kwao kwa kuifanyia kazi ni katika hekima zilizotakiwa.
  • Katazo la kubusu vitu ambavyo sheria haikusema kuwa tuvibusu kwa lengo la kuviabudu, kama mawe na mengineyo.
explain-icon

Ziada