explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hatoingia motoni aliyehudhuria vita vya Badri vilivyotokea katika mwaka wa pili wa Hijiria (kalenda ya kiislamu) akipigana pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wala aliyehudhuria suluhu ya Hudaibia, na ndani yake kukiwa na uungaji mkono wa ridhaa (Baiatu ridhiwani) uliotokea katika mwaka wa sita wa Hijiria.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hapa kuna fadhila ya watu wa Badri na Hudaibia, na kwamba wao hawatoingia motoni.
  • Kumebainishwa kwamba Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya dhulma zao, na kuwawezesha kufa katika imani, na kuwaingiza peponi pasina kutanguliwa na adhabu ya moto, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.