explain-icon

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Abubakari na Omari radhi za Allah ziwe juu yao ndio watu bora baada ya Mitume na Manabii.
  • Peponi hakuna mtu wa makamo, bali atakayeingia atakuwa ni kijana wa miaka thelathini na tatu (33), na makusudio yake wao ndio mabosi wa kila mtu aliyekufa katika umri wa makamo duniani, au hilo ni kulingana na jinsi walivyokuwa katika dunia wakati wa kuzungumzwa kwa hadithi hii.