explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu hupata wivu na huchukia na hukarahika, kama ambavyo muumini hupata wivu na huchukia na kukarahika, nakuwa sababu ya wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa machafu kama zinaa liwati (Ushoga na ubasha) wizi na kunywa pombe na mengineyo katika machafu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kutahadhari na hasira na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake pale yanapofanywa maharamisho yake.