Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani watayaandika: Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k. Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.