explain-icon

Ufafanuzi

Alitakwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake awaombee washirikina dua mbaya kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Hakika mimi sikuagizwa na Mwenyezi Mungu na sikutumwa kuwa mtoa laana na kuwaombea watu kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na niwakatie heri, mimi sikutumwa kwa hayo, bali nilitumwa niwe sababu ya heri na rehema kwa watu wote, na kwa waumini hasa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Ukamilifu wa tabia zake rehema na amani ziwe juu yake.
  • Umuhimu wa kuusafisha ulimi kutokana na laana kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Hapa kuna katazo la kutoa laana.
  • Himizo la kuwahurumia watu.