explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kwamba watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kula milo miwili kwa siku moja isipokuwa mlo mmoja kati ya hiyo utakuwa ni tende.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wa nyumba yake, huenda kuna wakati hawakupata mlo zaidi ya mmoja.
  • Tende ilikuwa rahisi kwao kuliko chochote.
  • Ubora wa kuipa nyongo dunia na kutosheka na kichache katika maisha, na kuwa hilo ni katika tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana wa Mitume.
  • Kula milo miwili kwa siku ni katika mambo halali na yanayofaa, nayo ni katika desturi za Waarabu inafahamika, walikuwa wakila kwa siku milo miwili, chakula cha mchana, na chakula cha usiku.