explain-icon

Ufafanuzi

Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Inapendeza kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwisho wa chakula.
  • Kuna ubainifu wa fadhila kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kwa kuwa amewaruzuku na kuwasahilishia riziki, na akalifanya hilo kuwa ni kafara ya kusamehewa madhambi.
  • Mambo ya waja yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa uwezo wao au nguvu zao, na mja ameamrishwa kufanya sababu.