Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake tofauti kati ya yule anayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kati ya yule asiyemtaja, kuwa ni mfano wa tofauti iliyopo kati ya aliyehai na aliyekufa katika manufaa yake na uzuri wa muonekano wake, hivyo mfano wa yule anayemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai ambaye muonekano wake umependeza kwa kuwa na nuru ya uhai, na anamanufaa, na mfano wa yule asiyemtaja Mwenyezi Mungu ni mfano wa maiti ambaye muonekano wake umeharibika, na ndani yake kumebatilika, na hana manufaa ndani yake. Na vile vile nyumba inasifiwa kwa sifa ya kuwa hai endapo wakazi wake wanamtaja Mwenyezi Mungu, na vinginevyo itakuwa nyumba mfu kwa kubweteka wakazi wake na kutomtaja Mwenyezi Mungu; na nyumba ikiitwa hai na maiti wanakusudiwa wakazi wa nyumba hiyo.